• slide-background





    UWSA SACCOS

    Chama cha Ushirika cha Akiba na Mikopo....

  • slide-background





    UWSA SACCOS

    WAJUMBE WA BODI YA UWSA SACCOS....

  • slide-background





    UWSA SACCOS

    WAJUMBE WA BODI YA UWSA SACCOS....

  • slide-background





    UWSA SACCOS

    Semina kwa wanachama wote

Mkopo wa Maendeleo

Katika aina hii ya mkopo, mwanachama ataweza kuchukua kiasi kisichozidi Shs. 30,000,000/=. Riba ni 1.5% kwa mwezi kwa njia ya riba punguzo (Reducing Balance Method). Marejesho ni kuanzia mwaka mmoja hadi miaka mitatu.

Mkopo wa dharura

Mkopo huu ni kiasi kisichozidi Tsh 3,000,000/= Riba ni 2.0% kwa mwezi kwa njia ya riba punguzo (Reducing Balance Method). Marejesho ni miezi sita.

Mkopo wa Elimu

Mkopo huu ni kiasi kisichozidi Tsh 3,000,000/= Riba ni 2.0% kwa mwezi kwa njia ya riba punguzo (Reducing Balance Method). Marejesho ni kuanzia mwaka mmoja had miaka miwili.

Mkopo wa Chap Chap

Mkopo huu ni kiasi kisichozidi Tsh 100,000/= Riba ni 5.0% kwa mwezi. Marejesho ni mwezi mmoja. Mkopo huu hutolewa wakati wowote pindi mwanachama anapohitaji

Mkopo wa Sikukuu

Mkopo huu ni kiasi kisichozidi Tsh 100,000/= Riba ni 5.0% kwa mwezi. Marejesho ni mwezi mmoja. Mkopo huu hutolewa kwa sikukuu zinazotambulika kiserikali

about-image
Kuhusu UWSA SACCOS

Kuhusu Chama

UWSA SACCOS LTD ni Chama cha Ushirika cha Akiba na Mikopo kilichosajiliwa kwa namba 914MBR. Chama hiki kilianzishwa mahususi ili kusaidia watumishi waajiriwa wa Mamlaka ya Majisafi na usafi wa Mazingira Mbeya.

Chama hiki kina jumla ya Wanachama 148 ikiwa wanaume ni 88 na wanawake ni 60 wenye jumla ya Hisa zenye thamani ya Shilingi 62,315,000/=.

Hadi kufikia mwaka 2022, Chama kimekuza mtaji wake hadi kufikia Shilingi Milioni 350 ikiwa ni mjumuisho wa Hisa na Akiba za Wanachama.

Soma Zaidi

DIRA NA DHIMA YA CHAMA

Mamlaka ya Chama yanatokana na Sheria ya Vyama vya Ushirika Na. 6 ya mwaka 2013 na Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha Na. 10 ya mwaka 2018 na Kanuni zake. Chama kilianzishwa ili kukuza maslahi ya kiuchumi ya chama na Wanachama

DIRA

Dira ya Chama ni; Kuwa Chama bora cha akiba na mikopo chenye kutoa huduma bora na riba nafuu kwa Wanachama,...

Soma Zaidi
DHIMA

Dhima ya Chama ni; Kutoa huduma bora ya utunzaji wa akiba za Wanachama, kutoa mikopo kwa Wanachama na kutoa elimu,...

Soma Zaidi
MISINGI YA CHAMA

Misingi ni suala la muhimu wakati wa kusimamia shughuli za Chama kwani husaidia kufikia malengo ya chama,...

Read More
MALENGO YA CHAMA

Malengo makuu ya Chama ni pamoja na:-

Kuhamasisha uwekaji wa akiba, hisa na amana ili kuendeleza na kukuza mtaji wa chama.

Kutoa elimu kwa jamii nzima ili kujua umuhimu wa kujiunga na UWSA SACCOS.

Kujengea uwezo Wanachama kwa kutoa mikopo yenye riba nafuu ili kuwainua kiuchumi.

Kutoa elimu kwa Wanachama ihusuyo bidhaa za Chama.

Soma Zaidi
about-image
Mawasiliano

Wasiliana nasi kwa maelezo zaidi

Barua Pepe : info@uwsasaccos.co.tz
Namba za Simu : 0785481977,   0677052800